Korea Kaskazini imefyatua kombora jingine la masafa ya kati juu ya anga la Japan na kuangukia katika Bahari ya Pasifiki, likisafiri kwa muda mrefu zaidi kuliko yote yaliyotangulia na likitajwa kuwa ishara ya ukaidi.
Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe amesema kuwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linapaswa kutoa ujumbe wa wazi kwa Korea kaskazini kutokana na kitendo hicho cha uchokozi.
Aidha, tangu Rais wa Marekani, Donald Trump alipoitishia kuishambulia Korea kaskazini mwezi Agosti mwaka huu, nchi hiyo imekwishafanya jaribio lake kubwa la kinyuklia, huku ikitishia kukishambulia kisiwa cha Guam na kufanya majaribio ya makombora mawili ambayo yanaruka kwa masafa ya mbali zaidi kupitia anga ya mshirika wa Marekani ambaye ni Japan.
Vile vile, Jopo la wakuu wa vikosi vya majeshi ya Korea kusini limesema kombora hilo liliruka kwa kiasi cha umbali wa kilometa 3,700 na kufikia kima cha juu kabisa cha kilometa 770 kwenda juu.
-
Wanamgambo 6 wa Al-Shabaab wauawa
-
Korea Kaskazini yatishia kuigeuza Marekani kuwa mavumbi, kuizamisha Japan
-
Urusi, Belarus zaanza mazoezi ya kijeshi
Hata hivyo, pamoja na kuwekewa vikwazo, Korea kaskazini imeapa kuendelea na majaribio yake kutokana na kile inachokiita uhasama wa Marekani dhidi yake, ikimaanisha uwepo wa maelfu ya wanajeshi wa Marekani katika nchi ya Japan na Korea Kaskazini.