Baada ya kuteuliwa kuwa kocha mpya wa Crystal Palace Roy Hodgson ameripotiwa kumtaka kiungo wa Arsenal, Jack Wishere ili kuhimarisha kikosi chake katika dirisha la usajili mwezi Januari.

Hodgson ambaye aliwahi kuwa kocha wa timu ya taifa ya Uingereza alikubali kuinoa Crystal Palace baada ya kutimuliwa kwa kocha Frank de Boer aliyeiongoza timu hiyo katika michezo minne ya ligi kuu ya Uingereza msimu huu.

Mkataba wa sasa wa Wilshere unamalizika mwishoni mwa msimu huu na kocha Roy Hodgson atamwangalia kwa ukaribu kiungo huyo wa kimataifa wa Uingereza mpaka mwaka mpya kabla ya kuamua kumsajili au vinginevyo.

Welshere amabye amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara alicheza kwa mkopo katika klabu ya Bournemouth msimu uliopita akianza vizuri na baadae kuvunjika mguu katika mchezo dhidi ya Tottenham.

Kama Jack Wilshere atashindwa kuingia katika mipango ya kocha Arsene Wenger msimu huu kiungo anaweza kumshuhudiwa akikipiga katika uwanja wa Selhurst Park unaomilikiwa na Crystal Palace.

 

 

 

Korea Kaskazini yafyatua kombora jingine, Japan yalalama
Majaliwa aungana na JPM kumuombea Lissu