Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema anaungana na Rais Magufuli, viongozi wengine na wananchi, katika kumuombea Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Antiphas Lissu aliyepigwa risasi.

Ameyasema hayo hii leo bungeni mjini Dodoma alipokuwa akisoma hotuba ya kughailisha bunge, ambapo amesema kuwa anamuombea Tundu Lissu ili aweze kupona na kurejea katika hali yake ya kawaida na kwenye shughuli zake kwa jamii.

“Naungana na Mh. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, Spika wa Bunge Job Ndugai, wabunge na wananchi mbali mbali, kumpa pole kwa majeraha na maumivu makubwa anayoyapata, na tunamuombea apone haraka na kurejea kwa familia yake.

Aidha, Majaliwa amesema anamuombea mbunge huyo apone haraka zaidi ili aweze kurejea bungeni kuendelea na majukumu yake ya kila siku ya kuwatetea na kuwasaidia wananchi wanaohitaji huduma yake.

Hata hivyo, Majaliwa ameghailisha shuguli za bunge kwa mujibu wa sheria mpaka ifikapo Novemba 7 mwaka 2017 litakapoanza vikao vyake tena kwa mara nyingine.

Roy Hodgson amnyemelea Wilshere
Wazee wa Kigoma wamjia juu Spika Ndugai