Korea Kaskazini imeendelea na majaribio yake ya silaha za nyuklia huku kwa sasa ikifyatua baharini makombora kadhaa ya masafa mafupi kutokea pwani ya mashariki ya nchi hiyo.
Korea Kaskazini imeendelea na majaribio yake ya silaha hizo wakati Marekani na Korea Kusini wakifanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi ya kila mwaka ambayo Korea Kaskazini imesema kuwa ni maandalizi ya vita.
Aidha, kituo cha Jeshi la Marekani katika ukanda wa Pasifiki kimesema kuwa kimegundua kuwa makombora matatu ya masafa mafupi yaliyofyatuliwa ndani ya kipindi cha dakika 20. na yote yalifeli.
Hata hivyo, Makao makuu ya Jeshi la Korea Kusini limesema kuwa majaribio hayo yamefanywa kutokea mashariki mwa Korea Kaskazini yakaruka katika upande wa Kaskazini mashariki karibu kilomita 250 kuelekea baharini