Korea kaskazini imeendelea na mpango wake wa kuunda makombora mapya licha ya kuidhinisha uhusiano mwema na utawala wa rais Donald Trump.
Satelaiti za kijasusi za Marekani zimegundua shughuli zinazoendelea katika eneo ambako kumetengenezwa makombora ya masafa marefu.
Aidha, Shirika la habari la Reuters limemnukuu afisa mmoja wa kijasusi wa Marekani akisema kuwa haijajulikana wazi ni kwa kiwango gani shughuli hiyo imeendelea.
Hata hivyo, hizi sio taarifa za kwanza kuwa Korea Kaskazini huenda inaendelea na uundaji wa mpango wake wa silaha, na kutilia shaka athari halisi ya mkutano wa Singapore.
-
Mkuu wa Majeshi Iran amvaa Trump, ‘anzisha tumalize’
-
Mkurugenzi Mkuu CBS achunguzwa kwa kashfa ya ngono
-
Mnangagwa amnyang’anya Mugabe walinzi