Rais wa Marekani Donald Trump amefanya mazungumzo kwa mara ya kwanza na Rais wa Korea Kusini kuhusu majaribio mbalimbali ya silaha za nyuklia yanayofanywa na Korea Kaskazini.
Katika mazungumzo hayo, Trump amesema kuwa amefurahishwa na hatua zilizochukuliwa na Baraza la Usalama la umoja wa Mataifa wa kuiwekea vikwa vya kiuchumi Korea Kaskazini dhidi ya mpango wake wa majaribio ya silaha za nyuklia.
Aidha, taarifa zaidi zimesema kuwa waziri mkuu wa Korea Kaskazini naye amefanya mazungumzo na waziri mwenzie kutoka Korea Kusini kwenye mkutano wa masuala ya usalama nchini Philippines.
Hivi karibuni waziri wa mambo ya nje wa Korea Kusini alisema kuwa milango iko wazi kwa Korea Kaskazini endapo itahitaji kufanya mazungumzo ili kuweza kutafuta ufumbuzi wa mgogoro uliozikumba nchi hizo.
Hata hivyo, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeiwekea vikwazo vya kiuchumi Korea Kaskazini dhidi ya mpango wake wa kufanya majaribio ya makombora ya masafa marefu ambayo yamekuwa ni tishio.