Baraza la usalama la Umoja wa mataifa, limechukua hatua kali ya kuiadhibu Korea Kaskazini dhidi ya mpango wake wa majaribio ya silaha za masafa marefu na za nyuklia ambazo zimekuwa tishio la usalama katika nchi jirani.

Katika kura ya pamoja, baraza hilo limeidhinisha vikwazo vipya, vinavyolenga biashara ya chuma na makaa ya mawe yanayotoka Korea Kaskazini na kuuzwa nchi za nje, bidhaa ambayo huiingizia dola bilioni moja kwa mwaka.

Aidha, kwa upande wake Rais wa Marekani, Donald Trump amezipongeza hatua za China na Urusi za kuunga mkono vikwazo hivyo vilivyotolewa na baraza hilo la Umoja wa mataifa, huku akisema kuwa vikwazo hivyo vitakuwa na athari kubwa katika biashara ya nchi hiyo.

Hata hivyo, Korea Kusini, imeiomba Korea Kaskazini kutenga muda ili wafanye mazungumzo kuhusu mgogoro uliopo baina nchi hizo mbili kuhusu mpango wa wa Korea Kaskazini wa utengenezaji silaha za nyuklia.

 

 

LIVE: Rais Magufuli akizindua Kiwanda cha Saruji jijini Tanga
Magazeti ya Tanzania leo Agosti 6, 2016