Miaka 24 imepita tangu kuzama kwa meli ya MV Bukoba, Mei 21, 1996, MV Bukoba ilipokuwa inakaribia bandari ya Mwanza umbali wa kilometa 56, ilizama kimo cha meta 25 majini, hivyo kusababisha vifo vya watu 894.
Hata hivyo, yamekuwepo makisio ya vifo kuweza kufikia watu 1,000, kwa sababu kulikuwa na idadi ya abiria ambao hawakusajiliwa, vilevile kuna miili ambayo ilishindikana kuiopoa.
Meli hiyo iliundwa mwaka 1979 ikiwa na uwezo wa kubeba mizigo tani 850 na abiria 430 iliyokuwa ikitoa huduma ya kubeba mizigo na abiria ndani ya Ziwa Victoria kati ya Bandari za Bukoba na Mwanza.
Picha ya zamani ya Rais yamtia mbaroni Idriss Sultan
Kinyume na uwezo halisi wa meli, Ilikadiriwa kwamba abiria zaidi ya 2,000 walikuwemo kwenye MV Bukoba ilipokuwa ikipata ajali.
Kikubwa cha kukumbukwa kuhusiana na MV Bukoba ni meli hiyo kutokuwa na majaketi ya uokovu, vilevile maarifa kidogo ya uokoaji. Uamuzi wa kukata sakafu ya meli iliyokuwa imepinduka juu chini, uliizamisha meli zaidi, hivyo kuondoa matumaini ya kuokoa watu waliokuwa hai wakilia na kugonga meli.