Mbunge wa Jimbo la Ubungo kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Saed Kubenea amezua mjadala baada ya kudaiwa kuandika barua ya kuomba kujiuzulu.

Kubenea anadaiwa kuandika barua kuomba kujiuzulu nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, jambo ambalo linaonekana kuleta mgongano na kurushiana mpira.

Wakati mjadala huo ukishika kasi hadi sasa mbunge huyo hajakubali wala kukataa kuhusu barua hiyo aliyomwandikia Katibu Mkuu wa Chadema, Dkt. Vicent Mashinji ambaye amesema pindi itakapomfikia ataifanyia kazi haraka.

Aidha, barua hiyo ya Agosti 28 mwaka huu ilianza kusambaa mitandaoni juzi, ambapo Kubenea alikuwa akitoa utetezi wake kutokana na kuandikiwa barua na Katibu Mkuu wa chama hicho akitakiwa kujieleza kwanini asichukuliwe hatua za kinidhamu kwa kusababisha migogoro kupitia mitandao ya kijamii.

Katika barua hiyo yenye kumbukumbu MB/U/CDM/018/1  kwenda Ofisi ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Kubenea alitakiwa kujibu tuhuma tano dhidi yake.

“Barua hiyo kama ambavyo umesema mwandishi ipo mitandaoni mimi bado sijaiona na kama nikiiona nitaifanyia kazi,’’ amesema Dkt. Mashinji.

Hata hivyo, katika kile kinachooneka kuwa ni kukosekana kwa ufafanuzi wa kina Kubenea alikiri kupokea barua kutoka kwa Katibu Mkuu wa chama hicho ikimtaka kujieleza  kutokana na kikao cha Kamati Kuu (CC) iliyokutana Julai 7 na 8 mwaka huu.

 

Bobi Wine avutana na balozi wa Uganda nchini Marekani
CUF wakoleza wino wa Chadema kumtaka Maalim Seif Urais 2020