Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa namba maalumu ya kubonyeza kwenye simu ambayo itamuwezesha mtumiaji wa simu kufahamu kama kitambulisho chake cha Taifa kimetumika kusajili namba ya simu ambayo haifahamu.
TCRA imetoa namba hiyo baada ya kuwepo na baadhi ya mawakala ambao si waaminifu kutumia kitambulisho cha mtu kusaliji namba zaidi ya moja kwa kutumia jina lako bila wewe mhusika kufahamu ambapo laini hizo ndizo zinazotumika kufanya uhalifu.
Piga *106# kuhakiki usajili wa laini yako leo na ungalie kama namba za kitambulisho chako cha Taifa zimetumika kusajili namba za simu usizozifahamu.
Njia ya kwanza ya kujiweka salama ni kuhakiki kujua wasifu wa kitambulisho chako cha Taifa kwa kubonyeza *106# na kisha utakutana na hatua mbalimbali, hii inasaidia kufahamu matumizi ya kitambulisho chako katika usajili wa simu.