Uyoga unapatikana baada ya kuozesha kwa baadhi ya mimea, baada ya mchakato huo ndipo huota ukiwa na rangi tofauti kutokana na aina ya mimea kwa ujumla chakula hiki kina ladha kama kuku wa kienyeji hivyo kumfanya mlaji kula kwa furaha.
Ndani ya uyoga kuna virutubisho muhimu ambavyo hukinga mwili na kuuponya na maradhi mbalimbali.
Kwa mujibu wa watafiti wa afya wamethibitisha kuwa uyoga unautajiri wa vitamini B2, B3, B5, B6, na B Complex ambayo husaidia kuondoa mafuta ‘kolestro’ katika mwili pamoja na kinga dhidi ya maradhi.
Baadhi ya magonjwa ambayo yanathibitiwa endapo utakula uyoga ni pamoja na shinikizo la moyo, kiharusi pamja na moyo kusimama ghafla.
Vilevile katika uyoga kunapatikana kiwango kikubwa cha madini ya Zinc ambayo husaidia kuimarisha kinga za mwili na kuimarisha kiwango cha sukari mwilini, unashauriwa kula uyoga walau mara moja kwa mwenzi ili kuimarisha afya yako