Kwamujibu wa ripiti iliyotolewa Juni 10, 2019 na JAMA International Medicine, kwa mara ya kwanza kabisa kuwahi kutolewa duniani inaeleza uhusiano kati ya kuongezeka kwa uzito wa wanawake na kulala kwenye vyumba vyenye mwanga mbadala (usio wa jua).
Ripoti hiyo imewatahadharisha wanawake kuhusu kulala kwenye vyumba vyenye mwanga wa taa au mwanga wowote ule wa televisheni nyakati za usiku huongeza nafasi ya kuongezeka na kupata vitambi.
Ripoti hiyo inawashauri wanawake kulala kwenye vyumba vilivyozimwa taa yaani kulala gizani ili kuepukana na tatizo hilo.
Sehemu ya ripoti inaeleza ” Binadamu ameumbwa akizungukwa na mifumo ya mwanga wa jua nyakati za mchana na giza wakati wa usiku hivyo mwili kupata mwanga usiku kunaweza kubadili mfumo wa utendaji kazi wa homoni pamoja na mifumo mingine shirikishi”
Hata hivyo ripoti hiyo haijaeleza kwanini athari hii inawapata wanawake tu, sababu halisi ya kutokea pamoja na utaratibu mzima wa namna ambavyo jambo hilo linafanyika.