Kiongozi wa kundi la kigaidi lilalojiita Islamic State of Iraq and Syria (ISIS), Abu Bakr al-Baghdad anasadikika kuwa ameuawa katika shambulizi la kushtukiza lililofanywa na makomando wa Marekani, Jumamosi usiku, Oktoba 26, 2019 katika eneo moja nchini Syria.

Hata hivyo, Marekani inafanya uchunguzi kwa kutumia vipimo vya Vinasaba (DNA) ili kuthibitisha kwa uhakika taarifa hizo. Inaelezwa kuwa kiongozi huyo alivaa bomu la kujitoa muhanga na kwamba huenda alijilipua ili asiweze kukamatwa na makomando wa Marekani, hatua inayoelezwa kuwa kama ni kweli italeta changamoto ya utambuzi wake.

Kwa mujibu wa chanzo kimoja kilichoieleza CNN, Shirika la Kijasusi la Marekani (CIA) ndilo lililosaidia kupata maficho ya al-Baghdad.

Bado Serikali ya Marekani imeendelea kusita kutoa tamko la moja kwa moja kuhusu taarifa hizo kwani mwaka 2014 pia iliwahi kudaiwa kuwa ameuawa lakini Aprili mwaka huu alijitokeza na kutoa ujumbe kwa njia ya mkanda wa video kwa wafuasi wake.

Msemaji kutoka Makao Makuu ya Ulinzi wa Marekani ameiambia CNN kuwa wanaamini wamemuua lakini hawawezi kutoa uthibitisho hadi watakapopata majibu ya DNA.

Kulala bila kuzima taa husababisha vitambi kwa Wanawake
Video: Membe avuruga serikali, CCM, JPM amedhamiria kweli