Mara baada ya aliyekuwa Diwani wa kata ya Vingunguti, Naibu Meya Manispaa ya Ilala kupitia tiketi ya Chama cha Wananchi CUF, Omary Kumbilamoto kujiudhuru amesema ugomvi unaoendelea ndani ya CUF ni kama mgogoro wa Israel na Palestina akidai kuwa mgogoro huo hauna suluhu.
Hivyo ameamua kujivua uongozi huo katika chama hicho ili awe huru mara baada ya kudai kuwa amekuwa akipokea vitisho kutoka kwa viongozi wa chama hicho wakati akiunga mkono serikali katika kutekeleza majukumu ya kuwatumikia wananchi.
“Nimejivua uanachama wa CUF na nafasi zangu zote ndani ya chama ikiwemo ya udiwani katika kata ya Vingunguti pia unaibu meya wa manispaa na nimechukua hatua hii ili kulinda na kutetea maslahi ya wananchi ninaowatumikia hivyo ili niendelee kuteleza majukumu yangu ipasavyo najivua ili kuunga mkono jitihada za rais Magufuli na viongozi wote Serikali kwa ujumla” amsema Kumbilamoto.