Deni la jumla la taifa la Amerika lilizidi hadi $31 trilioni kwa mara ya kwanza, hatua ambayo inatajwa kuwa ni mbaya na yenye hali tete ya kiuchumi kwa taifa hilo tajiri Duniani.
Viwango vya chini vya riba vya kihistoria, vimekuwa vikibadilishwa na gharama kubwa za kukopa zikiwekwa huku Hifadhi ya Shirikisho nchi hiyo ikijaribu kukabiliana na mfumuko wa bei kwa haraka.
Wawekezaji nchini Marekani, sasa wanahama taasisi za fedha kutokana na hofu ya kushuka kwa uchumi duniani na tayari masoko ya Marekani yamengezeka na kupanda kwa zaidi ya asilimia 3, huku ripoti ya serikali ikionesha dalili za kupungua kwa soko la ajira.
Hata hivyo, wawekezaji hao wamelichukua jambo hilo kama ishara ya kiwango cha riba cha Fed kinaongezeka, ambacho kinatokana na gharama za kukopa kwa makampuni, na hivi karibuni kinaweza kuanza kukua taratibu.