Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewaapisha Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar (DPP), Mgeni Jailani Jecha, Mrajisi wa Mahakama Kuu Zanzibar, Valentina Andrew Katema na Naibu Mhasibu Mkuu wa Serikali ya Zanzibar, Shaheen Fauz Mohamed.

Hafla ya uapisho huo, hiyo imefanyika hii leo Oktoba 5, 2022 Ikulu mjini Zanzibar, na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Kitaifa, Vyombo vya ulinzi na usalama na Viongozi wa dini.

Akizungumza baada ya uapisho huo, Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar, Mgeni Jailani Jecha amesema kipaumbele chake katika utendaji wa nafasi hiyo ni kuhakikisha kesi za jinai hasa za udhalilishaji zinafanyiwa kazi.

Kwa upande wake, Mrajis wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, Valentina Andrew Katema amesema atahakikisha anasimamia misingi ya sheria na kanuni zinazomuongoza kwenye utendaji wa majukumu huku Naibu Mhasibu Mkuu wa Serikali ya Zanzibar, Shaheen Fauz Mohamed akisema atahakikisha anazisimamia fedha kwa uadilifu.

Mabingwa wa Burundi kucheza Azam Complex
Matumizi mabaya bidhaa za mbao kuleta athari Duniani