Mshambuliaji Habib Kyombo amaiokoa Simba SC kwa kufunga bao la kuasawazisha dakika ya 81 katika mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki dhidi ya Mabingwa wa Sudan Al Hilal ‘Omdurman’.

Mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es salaam, ulishuhudia Kyombo akifunga bao hilo baada ya kupokea Kross iliyopigwa kiufundi na Kiungo Mshambuliaji Pape Ousmane Sakho

Simba SC imelazimisha matokeo hayo baada ya kutanguliwa kufungwa bao la mapema dakika ya 16, likifungwa na Kiungo Mshambuliaji kutoka DR Congo Makabi Lilepo, akiunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na Ibrahim Imoro.

Mchezo huo ulikuwa wa mwisho kwa klabu hizo, kabla ya kuanza safari ya kwenda ugenini kucheza michezo ya Hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Simba SC itacheza mchezo wa Kundi C dhidi ya Mabingwa wa Guinea Horoya AC mjini Counakry katika Uwanja General Lansana Conte, Jumamosi (Februari 11).

Al Hilal itacheza mchezo wa Kundi B dhidi ya Mabingwa wa Afrika Kusini Mamelod Sundowns ‘Masandawana’ mjini Pretoria, Jumamosi (Februari 11).

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Februari 6, 2023
Tisa wakiwemo Viongozi wa siasa mbaroni kwa kulima bangi