Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini – LATRA, CPA Habibu Suluo amesema mamlaka hiyo ipo mbioni kutoa mwongozo kwa waendeshaji wa usafiri wa waya, ambao wanatarajia uwekezaji huo utafanyika zaidi katika sekta ya Utalii.

CPA Suluo ameyasema hayo leo Oktoba 19, 2023 katika kikao kazi chenye nia ya kutoa ufafanuzi na kuwajengea uelewa Wanahabari nchini chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina na kuongeza kuwa wataangalia ni namna gani ambavyo utakuwa na tija nchini hususani Sekta ya Utalii.

Amesema, “lengo ni kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan za kuinua Sekta ya Utalii hapa nchini, sisi hatuwekezi huko bali, sisi tunaweka miongozo, kanuni za udhibti wa usafiri huo.”

CPA Suluo ameongeza kuwa, wadau wa LATRA ni wasafirishaji wa mabasi ya njia ndefu na mabasi ya miji na majiji, magari ya mizigo, madereva wa mabasi na malori, wakiwemo watoa huduma wa magari maalumu ya kukodi, watoa huduma wa taxi mtandao, abiria, taasisi za umma pamoja na wananchi kwa jumla.

Kwa upande wake Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu amesema LATRA ni taasisi ya 20 ambayo ipo chini ya Ofisi ya Msajili wa Hazina na kusisitiza kuwa suala la utawala bora katika mashirika hayo ni jambo muhimu na ambalo halikwepeki.

“Lengo la Serikali ni kuona mashirika hayo yanafikia lengo lake, ikisingatiwa kwamba yameanzishwa kwa mujibu wa sheria, mashirika haya kwa kiasi kikubwa yamefikia kiwango cha kuridhisha japo kuna machache ambayo hayajafikia malengo,” amesema.

Prince Dube: Hatutaingia kinyonge
Robertinho: Mzuka umeongezeka kambini