Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini – LATRA, imeongeza muda wa wiki mbili kwa wadau wa usafiri nchini, ili kuweza kutoa maoni yao katika kanuni za Mamlaka ya udhibiti usafiri ardhini za utaratibu wa kushugulikia malalamiko.

Mkurugenzi wa huduma za usafiri, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Sekta ya Uchukuzi, Mhandisi Aron Kisaka ameyasema hayo wakati wa mkutano wa kupokea maoni ya wadau kuhusu rasimu za kanuni mpya za mamlaka.

Amesema, kanuni zimechelewa kuwafikia wadau na siku bado hazitoshi kwa wadau wa usafiri kuweza kutoa maoni yao. Amewaomba wadau wa usafirishaji nchini waweze kutuma maoni yao kwa barua pepe ili isaidie katika ukusanyaji wa maoni.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa udhibiti wa Usafiri wa barabara kutoka LATRA, Johansen Kahatano amesema wataendelea na ukaguzi wa lazima wa vyombo vya usafirishaji Biashara kwa mwaka 2023 huku akiwashauri watumiaji wa usafiri kupanda mabasi yalio salama.

Muithiopia kuikamua Simba SC Milioni 300
Mapigano DRC yasababisha vifo vya raia 500