Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini – LATRA, imetangaza mabadiliko ya nauli katika safari za masafa marefu na masafa mafupi baada ya kupitia maoni ya wadau wa usafiri nchini.

Kwa mujibu wa LATRA, nauli za safari zisizozidi kilometa 10 ambayo nauli yake ilikuwa shilingi 500 sasa itakuwa 600 ambapo kwa safari za kilometa 11 hadi 15 ambayo nauli yake ilikuwa Shilingi 550 sasa itakuwa Shilingi 700.

Kwa kilometa 15 hadi 20 ambapo nauli ilikuwa Shilingi 600 sasa itakuwa 800 huku kwa safari za kilometa 21 hadi 25 nauli imetoka 700 hadi Shilingi 900 na kwa Safari ya kilometa 26 hadi 30 nauli ni shilingi 1100, safari ya kilometa 31 hadi 35 ni shilingi 1300.

Safari za Kilometa 36 hadi 40 nauli ni 1400 huku nauli za Wanafunzi zikiendelea kusalia Shilingi 200 kwa safari za masafa mafupi.

Dira maendeleo ya Taifa 2050: Tume ishirikishe Wananchi - Dkt. Biteko
Serikali yabainisha mikakati ustawi wa Walemavu