Lebanon wananchi wameandamana kuishinikiza viongozi wajiuzulu kutokana na mlipuko uliotokea katika bandari ya Beirut na kusababisha vifo vya watu 157 na kujeruhi wengine 5,000
Madhara ya mlipuko huo huenda yakaongezeka kwa kuwa bado shughuli za uokoaji zinaendelea, tangu tukio hilo lilipotokea Agosti 5 huku ikiwa tayari imetangaza siku tatu za maombolezo ya Kitaifa
Raia wameandamana nchini humo kutokana na taarifa zibazosema kuwa huenda kilichosababisha mlipuko huo ni Ammonium Nitrate iliyokuwa imehifadhiwa ghalani na kuwa Serikali ilipuuza onyo la Wataalum kuiondoa ama ingelipuka
Mamlaka za Lebanon zimewakamata watu 16 huku uchunguzi zaidi wa tukio hilo ukiendelea.
Waziri wa Mambo ya Nje, Charbel Wehbe amesema wameunda baraza litakalochunguza tukio hilo kwa siku nne
Pia, maafisa waliopewa tahadhari ya kuiondoa Ammonium Nitrate katika bandari wamezuiwa kutoka majumbani mwao (home detention) ili kupisha uchunguzi