Shirikisho la Kimataifa la Historia na Takwimu za Mpira wa Miguu (IFFHS) limetangaza orodha ya Ligi Bora duniani kwa mwaka 2021, ambapo Ligi Kuu ya Brazil (Serie A) imeshika nafasi ya kwanza.
Taarifa za ‘IFFHS’ zimethibitishwa na Shirikisho la Soka nchini Tanzania ‘TFF’ kwa kuchapishwa kwenye kurasa rasmi za mitandao ya kijamii za shirikisho hilo leo Alhamis (Februari 03).
Katika orodha hiyo Ligi Kuu Tanzania Bara imepanda kwa nafasi tisa (9) kutoka nafasi ya 71 (2020) hadi nafasi ya 62 (2021) duniani huku kwa Bara la Afrika ikishika nafasi ya 10 na kusalia kuwa Ligi pekee kwenye 10 Bora ya Afrika kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Kwa upande wa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ‘CECAFA’ Ligi Kuu Tanzania Bara inashika nafasi ya kwanza.