Waliowahi kuwa mabingwa wa michuano ya klabu bingwa barani Ulaya Benfica, Ajax na Red Star Belgrade wamefanikiwa kufuzu kucheza hatua ya mwisho ya mtoano kwa msimu wa 2018/19, baada ya kupata ushindi wa jumla katika michezo ya kuwania kufuzu hatua hiyo usiku wa kuamkia leo.
Mabingwa wa 1961 na 1962 SL Benfica, wamesonga mbele na kutinga hatua ya mwisho ya mtoano, kufuatia ushindi wa mabao mawili kwa moja walioupata dhidi ya Fenerbahce, ambao ulitanguliwa na matokeo ya sare ya bao moja kwa moja iliyopatikana juma lililopita mjini Istanbul.
Mabingwa mara nne wa michuano hiyo (1970–71, 1971–72, 1972–73, 1994–95) Ajax Amsterdam nao wamesonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao matano kwa mawili dhidi ya Standard Liege.
Red Star Belgrade, mabingwa wa mwaka 1991, nao walifanikiwa kuifunga Spartak Trnava mabao mawili kwa moja 2-1 katika muda wa kawaida, na kuongezewa muda wa dakia 30 ambao uliwasaidia kuchomoza na ushindi wa mabao matatu kwa mawili.
Matokeo ya mchezo mingine ya kuwania kufuzu hatua ya mwisho ya mtoano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya iliyochezwa usiku wa kuamkiia leo.
Dynamo Kyiv 2 – 0 Slavia Prague
BATE Borisov 1 – 1 Qarabag FK
Spartak Moscow 0 – 0 PAOK Thessaloniki FC
AEK Athens 2 – 1 Celtic
Dinamo Zagreb 1 – 0 FC Astana
Vidi FC 0 – 0 Malmoe FF
KF Shkendija 0 – 1 Salzburg
Spartak Trnava 1 – 2 FK Crvena Zvezda
Michezo ya mkondo wa kwanza na ya pili ya hatua ya mwisho ya mtoano, imepangwa kuchezwa Agosti 21,22,28 na 29.
Red Star Belgrade v Red Bull Salzburg
BATE Borisov v PSV Eindhoven
Young Boys v Dinamo Zagreb
MOL Vidi v AEK Athens
Benfica v PAOK
Ajax v Dynamo Kyiv