Mshike mshike wa ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu wa 2019/20 utaendelea tena leo usiku kwa michezo ya makundi manne kuchezwa katika viwanja tofauti.
Michuano hiyo inayoleta msisimko karibu duniani kote, imerejea kwa kishindo baada ya mashabiki kuanza kushuhudia vumbi likitimka usiku wa kuamkia leo kwa michezo ya makundi manne kuchezwa.
Kwa mshtuko mkubwa mabingwa watetezi Liverpool walianza vibaya kwa kufungwa mabao mawili kwa sifuri dhidi ya SSC Napoli, huku mabingwa wa soka nchini Hispania FC Barcelona wakilazimisha sare ya bila kufungana dhidi ya Borussia Dortmund.
Timu ya mtanzania Mbwana Samatta KRC Genk nayo ilianza vibaya michuano hiyo kwa kufungwa mabao sita kwa mawili, huku nahodha na mshambuliaji huyo wa Taifa Stars akifunga moja ya mabao ya kufutia machozi.
-
Jurgen Klopp ajitetea kwa kichapo, Ancelotti achekelea
-
Ross Barkley ajitwisha mzigo wa lawama, Lampard amtetea
Leo itakua zamu ya makundi A,B,C na D, baada ya kushuhudia michezo ya makundi E,F,G na H ikichezwa usiku wa jana.
Kundi A
Club Brugge Vs Galatasaray
Paris Saint-Germain Vs Real Madrid
Kundi B
Olympiacos Vs Tottenham Hotspur
FC Bayern Munich Vs FK Crvena Zvezda
Kundi C
Dinamo Zagreb Vs Atalanta
Shakhtar Donetsk Vs Manchester City
Kundi D
Atletico Madrid Vs Juventus
Bayer Leverkusen Vs Lokomotiv Moscow