Kuongezeka Majina haya ya Wachezaji wanaoitwa kwenye timu zao za Taifa na tena Mataifa yenyewe ni makubwa Kisoka yanafanya Ligi yetu izidi kujizolea Watazamaji na wafuatiliaji wapya kutoka kwenye Nchi husika.Lakini pia vilabu vinavyowamiliki wachezaji vinakuwa vinapata airtime ya Bure Kupitia hao Wachezaji ambao ni kama Mabalozi wao huko waliko.
Kupitia hili pia inaonesha namna gani Timu zetu zimeongezeka Ubora (Simba na Yanga zinazoshiriki Kimataifa).Kile kinachofanywa na Wachezaji hawa hasa kwenye Mashindano ya Kimataifa Mafanikio yake ndio yanaonekana kwa kuitwa kwa Wachezaji kwenye Mataifa yao.
Jambo la Msingi ni kuhakikisha vilabu vyenye Pesa za kusajili Wachezaji Bora vinakuwa vingi na pia ‘UPIGAJI’ upungue ili tuzidi kupasua anga na kuchukua nafasi ya baadhi ya Ligi zilizoanza kuchechemea.
Wachezaji wa kigeni wanaocheza Ligi Kuu Tanzania Bara ambao wameitwa katika Timu zao za taifa ni Clatous Chama, Kenedy Musonda, Stephanie Aziz Ki, Pape Osmane Sakho, Fiston Mayele, Henock Inonga Baka, Djigui Diarra, Saido Ntibanzokiza, Khalid Aucho na Peter Banda.
Imeandikwa na Abadan Kamwe Jr.