Imeelezwa kuwa kuondoka kwa Sergio Busquets ndani ya FC Barcelona ni hatua ya awali ya kurejea kwa aliyekuwa staa wa timu hiyo, Lionel Messi.
Busquets ametangaza kuondoka ndani ya FC Barcelona ifikapo mwisho wa msimu huu, baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa zaidi ya misimu 15.
Messi naye anatarajiwa kumaliza mkataba wake ndani ya Paris Saint-Germain ifikapo mwishoni mwa msimu huu.
FC Barcelona inapambana kuhakikisha inamrejesha Messi ndani ya kikosi hicho baada ya staa huyo kuondoka mwaka 2021.
Timu hiyo imekuwa ikipambana ndani ya La Liga kuhakikisha inafuata vizuri sheria kutokana na kukabiliwa na suala la kiuchumi kwani wanatakiwa kuweka kila kitu sawa ili kupata nafasi ya kumsajili staa huyo.
Rais wa La Liga, Javier Tebas amesema: “Kuondoka kwa Busquets ni mwanzo wa Messi kurejea, ingawa bado kuna vitu vingi vinatakiwa kufanyika, sio mimi ambaye natakiwa kuwaonesha wao njia, mpango wa kubana matumizi ya fedha kwao ndipo kuna shida.”