Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema kuwa baada ya Tundu Lissu kutolewa katika Kituo cha Polisi Kati leo mchana amepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kupimwa mkojo.
Mapema hii leo asubuhi, Mawakili akiwemo Fatma Karume walizuiliwa kuonana nae huku Jeshi la Polisi likisema litaendelea kumshikilia mpaka pale uchunguzi utakapokamilika ndipo litakapomuachia.
Aidha, Mbunge huyo wa Singida Mashariki na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika TLS alikamatwa jana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), akielekea Kigali Rwanda kwenye kikao cha Halmashauri ya EALS.
“Kabla ya kuelekea nyumbani kwake Tegeta, wamempeleka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali na ameshapimwa mkojo sasa sijui ni nini kinachochunguzwa, kwa sasa wameshaelekea kwake kwaajili ya kumpekua,”amesema Mrema
-
Video: Lissu afyatuka tena, anena mazito kuhusu JPM
-
Lowassa kitanzini tena, atinga kwa DCI kuhojiwa
-
Mbunge wa Jimbo la Temeke aswekwa rupango
Hata hivyo, ameongeza licha ya kulala rumande hakuna hata mmoja aliyeruhusiwa kuonana nae, wakiwemo wanasheria wake licha ya Fatma Karume na wengine Peter Kibatala na Fredrick Kihwelokuwepo kituoni hapo.