Mbunge wa Jimbo la Temeke Jijini Dar es salaam, Abdallah Mtolea amelala rumande tangu jana mara baada ya kukamatwa na Polisi kwa tuhuma za kuendesha gari ambalo bima yake ilikuwa imeisha muda mrefu.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Gilles Mrosso amesema kuwa mbunge huyo yuko rumande tangu jana jioni baada ya kukamatwa na askari wa usalama barabarani Temeke akiendesha gari ambalo bima yake ilikuwa imeisha muda mrefu.

“Askari wa usalama barabarani walipomhoji kuhusu kuendesha gari ambalo bima yake ilishaisha muda mrefu aliwapuuza na kuondoka hivyo walimfuatilia na kufanikiwa kumkamata na kumuweka ndani,”amesema Mrosso.

Hata hivyo, Kamanda Mrosso ameongeza kuwa taratibu za kumfikisha mahakamani zinafanyika kama sheria zinavyoelekeza kwa mtu yeyote ambae anakwenda kinyume na taratibu zilizowekwa.

Asilimia kubwa ya wanaume hawana nguvu za kiume
Ni huzuni kubwa, Mama Zari Hassan afariki dunia