Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu leo amesomewa mashtaka ya uchochezi na kurudishwa rumande akisubiri hatma ya dhamana yake.
Lissu alisomewa mashtaka ya kutoa lugha ya uchochezi dhidi ya Serikali, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbert Mashauri.
Mawakili watano wa upande wa Jamhuri waloshiriki katika kesi hiyo, wameiambia Mahakama kuwa Lissu alitenda kosa hilo la jinai Julai 17 mwaka huu katika eneo la Ufipa, Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Lissu ambaye alikuwa akitetewa na jopo la mawakili 20 wakiongozwa na Fatma Karume, alikana mashtaka dhidi yake. Mbunge huyo pia alisikika akisema, “kwakweli halijawahi kuwa kosa la jinai.”
Baada ya kusikiliza pande zote mbili Mahakama imeahirisha kesi hiyo hadi Julai 27 ambapo hatma ya dhamana ya mwanasiasa huyo ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) itakapojulikana.