Mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya Chadema, Tundu Lissu amefunguka na kuwashukuru Watanzania kwa maombi yao kufuatia oparesheni nyingine ya 19 ambayo amefanyiwa katika mguu wake.
Tundu Lissu alifanikiwa kufanyiwa oparesheni katika mguu wake wa kulia na kuisha salama, madaktari waliamua kufanya oparesheni hiyo kufuatia kugundua moja ya mfupa wake ulikuwa ukichelewa kuunga na kudai kuwa kama wasingefanya upasuaji na kurekebisha mfupa huo ungeweza kuchelewa zaidi na kuja kuvunjika baadae.
“Ninawashukuru kwa sala na maombi yenu” aliandika Tundu Lissu kupitia mtandao wake wa Instagram
Hata hivyo Watanzania mbalimbali wameendelea kumuombea Tundu Lissu ili aweze kupona haraka na kurudia tena katika hali yake ya zamani ili aweze kurudi nyumbani Tanzania na kuendelea na majukumu yake ya kila siku.
Tundu Lissu alishambuliwa kwa risasi mnano Septemba 7, 2017 na watu wasiojulikana akiwa mjini Dodoma na kisha baadae kupelekwa nchini Kenya kwa matibabu ambapo huku alifanyiwa oparesheni kadhaa katika mwili wake na baadae alikwenda nchino Beljium kwa matibabu zaidi ambapo jana amefanikiwa kufanyiwa oparesheni ya 19.