Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amepokea vituo sita vya polisi vinavyohamishika kwa ajili ya kuimarisha ulinzi na usalama katika Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, huku akibainisha kuwa eneo hilo lina matukio mengi ya uhalifu.
 
Masauni amepokea vituo hivyo mapema hii leo Kinondoni jijini Dar es salaa, ambapo Vituo hivyo vimetolewa na Kampuni ya vinywaji baridi ya CocaCola
 
Aidha, Masauni ameishukuru Kampuni hiyo kwa msaada huo uliolenga kuimarisha ulinzi na usalama na kuwataka wadau wengine kuiga mfano huo.
 
“Mipango yetu ya baadaye vituo kama hivi viwepo Dodoma Makao Makuu ya nchi ili kuimarisha ulinzi na usalama wa sehemu husika,”amesema Masauni.
 
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Jumanne Murilo amesema vituo hivyo vitawekwa katika maeneo ambayo hayana huduma za kipolisi na yenye changamoto za kihalifu.
 
  • Video: Prof. Bana awataka wanasiasa kutumia lugha zenye staha dhidi ya JPM
  • Video: JPM aishukia TRA, Tanzania yaandika rekodi mpya Afrika
 
  • Serikali yalivalia njuga tatizo la nguvu za kiume

Lissu atoa neno baada ya oparesheni ya 19
Urusi yaahidi kulipiza kisasi dhidi ya Uingereza