Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergey Lavrov amesema kuwa muda si mrefu Moscow itawafukuza wanadiplomasia kutoka Uingereza.

Urusi imefikia hatua hiyo mara baada ya Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May kutangaza kuwa ana mpango wa kuwafukuza wanadiplomasia 23 kutoka Urusi kufuatia kitendo cha jasusi wa zamani wa Urusi kupewa sumu.

Lavrov amesema kuwa hatua alioichukua May ni ya kijeuri na kusema imekusudia kupoteza lengo la hali ngumu ambayo inaikabili Uingereza katika kufanya mazungumzo ya kujiondosha Umoja wa Ulaya (EU).

Hata hivyo, Uingereza imesema kuwa imejiridhisha kuwa Urusi ilihusika na shambulizi hilo la sumu na Waziri Mkuu May ametangaza kuiadhibu Urusi kwa kuchukua hatua kadhaa, ikiwemo kuwafukuza idadi kubwa kuliko yoyote ile tangu 1971 ya wanadiplomasia wa Urusi wakati wa kipindi cha vita baridi.

 

Masauni apokea vituo 6 vya Polisi
Mhudumu aanguka kutoka kwenye ndege Uganda