Mhudumu wa ndege anadaiwa kuumia vibaya nchini Uganda baada ya kuanguka kutoka kwenye mlango wa dharura wa ndege shirika la Emirates.

Mwanamke huyo alikimbizwa hospitali akitokea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebbe, karibu na mji mkuu Kampala, baada ya kuanguka mlangoni siku ya Jumatano.

Ndege aina ya Boeing 777 ilitua muda mfupi kabla, na ilikuwa ikijiandaa kupokea abiria kabla ya kuelekea Dubai.

Mazingira ya kuanguka kwake yanaendelea kuchunguzwa, huku kukiwa na ripoti za mkanganyiko kuhusu tukio hilo.

Hata hivyo, shirika hilo la ndege limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, likiiambia Gazeti la Khaleej Times.

”Tunaweza kuthibitisha kuwa mmoja wa wafanyakazi wetu bahati mbaya alianguka kwenye mlango uliokuwa wazi wakati alipokuwa akiiandaa ndege ili kupandisha abiria.”

“Mfanyakazi huyo amepelekwa kwenye hospitali ya karibu. Tunatoa ushirikiano kadiri iwezekanavyo kwa mfanyakazi wetu, na kutoa ushirikiano zaidi kwa mamlaka zinazofanya uchunguzi.”

Urusi yaahidi kulipiza kisasi dhidi ya Uingereza
Jeshi la Polisi latoa ufafanuzi kuhusu mwili uliookotwa