Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA, Tundu lissu amesema uamuzi wake wa kufika Polisi Dodoma kujionea na kulichukua gari lake, haumaanishi kuwa hataki kesi dhidi yake iendelee.

Lisu ameyasema hayo hii leo Mei 9, 2023 mara baada ya kufika Polisi kwa ajili ya kukamilisha taratibu ili aweze kulichukua gari hilo na kuongeza kuwa kitendo hicho hakihusiani na kesi dhidi ya tukio lililomkuta.

Aidha, Lissu pia ametoa ufafanuzi kuhusu dereva wa gari lake wakati aliposhambuliwa Septemba 7, 2017 na kusema hajakimbia kesi bali alikua akitafuta salama yake na alipata usaidizi maalum akiwa nchini Kenya.

Akijibu swali la mwandishi kuu ya safari za mara kwa mara za kwenda ulaya, Lisu amesema hataacha kusafiki na kubainisha kuwa atakwenda tena na tena.

Dylan Kerr: Fiston Mayele ni mshambuliaji hatari
Jamie Carragher ampigia saluti Mo Salah