Watu 10 wamefariki, na wengine 40 kujeruhiwa wakiwemo Askari sita wa jeshi la zimamoto baada ya Lori la mafuta kulipuka katika mji wa Boksburg, uliopo eneo la mashariki mwa jiji la Johannesburg, nchini Afrika Kusini.
Lori hilo, lilikuwa likisafirisha gesi ya kimiminika (LPG), na lilipata hitilafu kisha kusimama chini ya daraja karibu na Hospitali na nyumba za raia siku ya Jumamosi Desemba 24, 2022 majira ya asubuhi.
Msemaji wa huduma za dharula William Ntlandi amesema, “Tulipokea simu kwa nambari 0750 ikituambia kwamba lori la mafuta lilikuwa limekwama chini ya daraja. Wazima moto waliitwa kuzima moto huo. Kwa bahati mbaya, lori hilo lililipuka.”
Amesema, mmoja wa waliojeruhiwa ni dereva ambaye amepelekwa hospitalini, na kwamba idadi ya vifo ilipanda hadi kufikia watu 10 kutoka vifo tisa viliyoripotiwa hapo awali huku nusu ya waliojeruhiwa, wakiwa katika hali mbaya na wengine 15 wakiwa na hali vizuri.