Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema anayeungwa mkono na vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa, Edward Lowassa amepiga kura katika jimbo la Monduli akiambatana na mkewe Regina Lowassa na kutoa mtazamo na matarajio yake.

Akiongea na waaandishi wa habari baada ya kukamilisha zoezi la kupiga kura, Lowassa alieleza kuwa ameshuhudia zoezi hilo likiendelea vizuri kwa utulivu katika kituo alichopigia kura na kuwataka watanzania wote kujitokeza kwa wingi kupiga kura.

“Kama bado wako nyumbani wajitokeze kwa wingi kabisa, hali hapa ni ya amani, wajitokeze kwa wingi kuamua hatma ya nchi yao” alisema Lowassa.

Akieleza kuhusu matarajio yake baada ya zoezi hilo kukamilika, Lowassa alisema kuwa anaamini kuwa atashinda katika uchaguzi huu, “natarajia ushindi”.

Hata hivyo, alieleza kuwa endapo itatangazwa vinginevyo, atakubali matokeo endapo mchakato utakuwa umefuata taratibu na haki imetendeka lakini kama taratibu, sheria na na haki haitatendeka hatakubali matokeo hayo.

 

 

Magufuli: Matone Ya ‘Mvua’ Yamenidondokea
Kingunge Atoa Maneno Mazito Kwa CCM Na Kikwete