Waziri Mkuu aliyejiuzuru na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa amesema kuwa bado hajawa na maoni juu ya mashinikizo kutoka sehemu mbalimbali ya kumtaka mwanae Freddy Lowassa kugombea ubunge jimbo la Monduli kwakuwa binafsi hayajamfikia.

Lowassa amesema kuwa maoni na mashinikizo ya mtoto wake kugombea jimbo la Monduli hayajamfikia hivyo hawezi kuzungumza chochote kwasasa.

“Mimi bado taarifa hizo za kumhusu Freddy sina, sijazipata. Ngoja kwanza nizifuatilie na baada ya hapo ninaweza kutoa tamko. Siwezi kuzungumzia kitu kwa sababu bado mimi hazijanifikia,”amesema Lowassa

Aidha, tangu kusambaa kwa taarifa za Mbunge wa jimbo hilo, Julius Kalanga kujiuzulu nafasi yake na kuhamia CCM jana usiku, mitandaoni kumekuwa na mashinikizo mbalimbali ambayo yakimtaka Freddy Lowassa  kugombea jimbo hilo.

Hata hivyo, Jimbo la Monduli limekuwa wazi kuanzia jana usiku baada ya Mbunge aliyechaguliwa mwaka 2015 (CHADEMA), Julius Kalanga kujiunga na CCM kwa kile alichoeleza kuwa ni kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. Magufuli na kudai kuwa ameondoka ndani ya chama hicho kwasababu ya siasa za chuki na uhasama.

Video: Usiombe kukutana na wanyama hawa
Olympic Marseille yajitosa kwa Olivier Giroud