Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amesema kuwa Watanzania hawana budi kujifunza kupitia tukio la ajali ya lori iliyopelekea vifo vya Watanzania zaidi ya 66.
Lugola ameyasema hayo mkoani Morogoro, ambapo amesema pindi ajali za namna hiyo zinapotokea, wananchi hawana budi kuviachia vyombo vya ulinzi na maafa kushughulika na masuala hayo.
“Tukio hili sio la kwanza kutokea na kujifunza, ila niseme Watanzania hatuna budi kujifunza, matukio ya namna hii yanayopotokea tuviache vyombo vya usalama na majanga ya ajali viendelee kushughulika, sisi wengine tukae pembeni,”amesema Lugola.
Aidha, Lugola amewaomba Watanzania kuendelea kuwa na utamaduni wa kuiheshimu sheria ya mitandao, na wao kama Serikali licha ya kukemea wataendelea kufuatilia watu wanaoendelea kuzisambaza picha zizizofaa mtandaoni.
-
LIVE MOROGORO: YANAYOJIRI MUDA HUU KATIKA ZOEZI LA KUITAMBUA MIILI 68 YA WALIOFARIKI AJALI YA LORI
-
Video: Ni msiba wa Taifa, Simanzi kwa Taifa, Inauma sana, Magufuli, Shein watuma salamu za rambirambi
-
Wizara ya Uchukuzi yanena kuhusu ajali ya Morogoro