Siku moja baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kulitaka Jeshi la Polisi kuwasilisha katika Ofisi za Bunge mkataba walioingia na mfanyabiashara anayemiliki Kampuni ya Lugumi Enterprises Ltd, Said Lugumi, mafanyabiasahara huyo ameripotiwa kutoroka nchini.

Lugumi anadaiwa kuingia mkataba huo na Jeshi la Polisi kwa ajili ya kusambaza mashine za kutambua alama za vidole katika vituo 108, lakini aliweka mashine hizo kwenye vituo 14 pekee huku akilipwa asilimia 90 ya kiasi cha mkataba, ambazo ni shilingi bilioni 34 kati ya bilioni 37 za mkataba husika.

Taarifa za kutoroka kwa Lugumi zimeripotiwa na gazeti la Mtanzania ambalo limedai kuzipata kutoka kwa baadhi ya maafisa wa vyombo vya dola nchini. Gazeti hilo limeeleza kuwa  kwa mujibu wa mafisa hao wa vyombo vya dola, Lugumi alitoroka Jumatatu ya wiki hii usiku, siku abayo Jeshi la Polisi lilitakiwa kuwasilisha mkataba huo kwa PAC.

Lugumi alikuwa na ulinzi mkali wa shirika binafsi la ulinzi na mara nyingi alikuwa akiongozana na msafara usio rasmi kumhakikishia ulinzi.

Jeshi la Polisi lilishindwa kuwasilisha Mkataba huo kwa PAC baada ya kupewa siku saba kwa njia ya mdomo, na sasa Kamati hiyo iliamua kutumia njia ya maandishi kwa kuliandikia barua jeshi hilo kuwasilisha mkataba huo katika Ofisi ya Bunge.

Julio: Waamuzi Walichezesha Kwa Maagizo Maalum Ya Kuibeba Yanga
ZFA Kuwapata Viongozi Wapya Hii Leo