Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Didier Gomes amesema kiungo kutoka nchini Uganda Tadeo Lwanga atakua sehemu ya kikosi chake kwenye mchezo wa kesho wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika, hatua ya Makundi.
Simba SC kesho Jumanne (Machi 16) itakuwa mwenyeji wa mchezo wa mzunguuko wanne wa ‘KUNDI A’ dhidi ya Al Merrikh kutoka Sudan, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.
Kocha Gomez amethibitisha kutarajia kumtumia kiungo huyo, akiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, ambapo alizungumzia maandalizi ya kikosi chake.
Amesema kiungo huyo atakuwepo, lakni atamkosa beki kutoka Ivory Coast Pascal Wawa,a mbaye alioneshwa kadi mbili za njano katika michezo miwiwli mfululizo, dhidi ya Al Ahly na kisha Al Merrikh.
“Tadeo Lwanga atacheza, Pascal Wawa ndio mchezaji ambaye atakosekana kwenye mchezo wa kesho lakini tunao wachezaji wengine wazuri ambao wanaweza kucheza nafasi yake kama Peter Muduhwa, Kennedy Juma au Erasto Nyoni na Ana Uzoefu Mkubwa.”
Lwanga aliibua sintofahamu ya kukosa mchezo wa kesho dhidi ya Al Merrikh, kufuatia kadi ya njano aliooneshwa kwenye mchezo uliopita mjini Khartoum Sudan, ambapo timu hizo zilitoka suluhu ya bila kufungana.