Wakati Dirisha Dogo la Usajili ilikifungwa Rasmi usiku wa kuamkia leo Jumatatu (Januari 16), Maafande wa Jeshi la Magereza ‘Tanzania Prisons’ wametangaza usajili wa wachezaji watano kwa ajili ya kuongeza nguvu klabuni hapo.

Tanzania Prisons ambayo ilimaliza mwaka 2022 kwa machungu ya kupoteza mchezo dhidi ya Simba SC kwa kufungwa 7-1, imetoa orodha ya wachezaji hao, ambao wanaamiwa watafanikisha mipango ya kufanya vizuri kikosini kwao.

Miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa Klabuni hapo yupo Meshack Selemani akitokea Nyasa Big Bullets ya Malawi, ambayo ilicheza dhidi ya Simba SC, katika hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika msimu huu 2022/23.

Wachezaji wengine waliosajiliwa Tanzania Prisons kupitia Dirisha Dogo la Usajili ni Mlinda Lango Benedict (Tinocco) amesaini Mkataba wa miaka miwili, Mohamed Ibrahimu (miaka miwili), Shabani -Kisiga (Mwaka mmoja) na Lambert Charlse Sabiyanka.

Wakati huo huo Tanzania Prisons imethibitisha kuachana na waliyokuwa wachezaji wao Hussein Abel ( Mlinda Lango) aliyesajiliwa KMC FC pamoja na Mudathir Abdallah aliyetimkia Ihefu FC.

Simba Queens yamrudisha Gaucho
Ripoti: 60 wauawa ndani wa wiki moja