Mshambuliaji Mwanahamisi Omary ‘Gaucho’ ametangazwa rasmi kurejea Simba Queens kupitia Dirisha Dogo la Usajili, ambalo rasmi limefungwa usiku wa kuamkia leo Jumatatu (Januari 16).

Simba Queens imethibitisha kumrejesha Mshambuliaji huyo, baadaya kuachana na Klabu ya Chabab Atlas Women FC ya nchini Morocco.

Klabu hiyo ilimsajili Mwanahamisi Msimu wa 2021/22, ambapo Mashabiki wengi walipongeza usajili wake, kwenda nje ya nchi, baada ya kuonesha uwezo mkubwa kisoka akiwa na Simba Queens.

Usajili wa Mshambuliaji huyo utaongeza chachu ya ushindani katika safu ya Ushambuliaji ya Simba Queens, ambayo kwa sasa inongozwa na Oppa Clement.

Shambulio la bomu Kanisani, 10 waaga dunia
Maafande wa Magereza wanasa chuma Nyasa Big Bullet