Kamati ya Maadili ya Tume ya Uchaguzi ya Zanziba (ZEC) imemsimamisha mgombea nafasi ya urais kupitia Chama cha ACT-Wazalendo ,seif Sharifu Hamad asifanye kampeni kwa siku tano.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Khamis Issa Khamis ametangaza uamuzi huo baada ya kamati hiyo ya Maadili ya ZEC kukutana na kujadili mwenendo wa kampezi za uchaguzi.
Khamis amesema Maalimu seif amekiuka sheria za kampeni na maadili.
kamati emeamua hivyo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa mgombea wa urais kwa chama cha Demokrasia Makini, Ameir Hassan ambae alilalamika kuhusu tabia ya Maalim Seif kuchochea wananchi kushiriki kura ya mapema ya Oktoba 27 ambayo ni mahususi kwa makundi maalumu, ambayo ni watendaji wa ZEC na wapiganaji wa vikosi vya ulinzi .
Alisema adhabu ya Mgombea huyo itaanza tarehe 16 Oktoba hadi Oktoba 20.