Waziri wa Afya wa Uganda, Jane Ruth Aceng amesema idadi ya waliothibitishwa kuwa na maambukizi ya ugonjwa wa Ebola nchini humo, imeongezeka na kufikia watu 109 huku 30 wakiripotiwa kufariki.
Aceng amesema, visa 15 vya maambukizi yaliyothibitishwa yamewajumuisha pia wahudumu wa afya sita, ambao tayari wamefariki kutokana na ugonjwa huo ulioikumba Uganda.
Amesema, kutokana na mazingira hayo kwasasa Serikali ipo katika harakati za kuanzisha kituo cha ziada cha matibabu, kitakachowezesha kutanua wigo wa upatikanaji wa huduma dhidi ya maradhi hayo.
Virusi vya Ebola, vinavyosambaa nchini Uganda ni aina ya kirusi kutoka Sudan, ambacho hakina chanjo iliyothibitishwa, tofauti na aina nyingine ya Ebola iliyopewa jina la Zaire, ambayo ilishuhudiwa wakati wa milipuko ya hivi karibuni katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.