Madaktari nchini Iran wamelaani hatua ya Polisi wa nchi hiyo, ya kuwatawanya kwa kuwarushia vilipuzi na mabomu ya machozi wakati wakiandamana kupinga uwepo wa vikosi vya usalama vituo vya kutolea matibabu na Hospitali.

Polisi hao, wanadaiwa kufanya tukio hilo Oktoba 27, 2022 wakati Madaktari hao pia wakiomboleza siku ya 40 ya kifo cha msichana Mahsa Amini, aliyefariki baada ya kukamatwa na Jeshi hilo akidaiwa kukiuka maadili na kanuni za mavazi ya dini (Hijab).

Madaktari hao, walisema kumekuwepo na ongezeko kubwa la vikosi vya usalama katika hospitali, ambako waandamanaji waliojeruhiwa wanakuwa wakipokea matibabu.

Awali, wanaharakati walisema vyombo vya usalama vilionya familia ya marehemu Mahsa Amini, kutofanya sherehe na kuwataka watu kutozuru kaburi la msichana huyo wa kikurdi, huku wakifunga barabara nyingi za mjini Tehrain.

Maambukizi ebola yafikia 109, Serikali yatoa tamko
Kimbunga Sitrang chaua watu 28