Idadi ya watu waliokufa kutokana na Kimbunga cha Sitrang nchini Bangladesh imefikia watu 28 huku huduma ya umeme ikikosekana katika sehemu kubwa iliyoathiriwa.

Idadi hiyo, imeongezeka baada wafanyakazi wa uokoaji wa Bangladesh kuipata miili ya wafanyakazi wanne waliotoweka kwa boti wakati wakifanya doria.

Kimbunga hicho cha Sitrang, kilipiga eneo la kusini mwa Bangladesh siku ya Jumatatu (Oktoba 24, 2022), huku Serikali ikisema karibu nyumba 10,000 na mazao ya  maeneo makubwa ya mashamba yakiharibiwa, wakati huu ambapo nchi hiyo inakabiliwa na mfumuko wa bei ya vyakula.

Vimbunga, vimekuwa ni janga na tishio la mara kwa mara katika eneo hilo, lakini wanasayansi wanasema huenda mabadiliko ya hali ya tabia nchi ikawa ni moja ya sababu ya kutokea mara nyingi kwa dhoruba hizo.

Madaktari walaani Polisi kuwarushia vilipuzi
Rais ataka changamoto za kitaasisi zishughulikiwe