Rais wa Kenya, William Ruto amefanya mabadiliko ya Baraza lake la Mawaziri kwa kuziunganisha Wizara mbalimbali na kuzibadili majina akisema yanalenga kuboresha utendaji kazi kama ilivyoainishwa katika ilani.

Katika mabadiliko hayo, Waziri wa mambo ya Nje, Alfred Mutua amehamishiwa Wizara ya Utalii na Wanyamapori, huku Waziri wa Biashara Moses Kuria akihamishiwa Wizara ya Utumishi wa Umma.

Rais wa Kenya, William Ruto.

Wizara ya mambo ya nje sasa itakuwa chini ya mamlaka ya Waziri Mkuu, Musalia Mudavadi na jumla ya Mawaziri wanane wamehamishwa Wizara na idara moja kuondolewa kutoka kwa afisi ya Waziri huyo Mkuu.

Rais Ruto pia amewateua Makatibu Wakuu kadhaa, Mabalozi na Manaibu wao, huku akiwahamisha wengine kuhudumu katika Wizara au Balozi mbalimbali.

Robertinho, Minziro Ng'adu kwa Ng'adu
Katumbi awasilisha ombi kugombea Urais DRC