Sheria ya huduma kwa vyombo vya habari iliyopitishwa wakati wa utawala uliopita ni miongoni mwa maeneo yanayotajwa kuminya uhuru na utendaji wa Waandishi wa Habari katika kutekeleza majumu yao.
Hatua hii, ilisababisha Jukwaa la Wahariri nchini Tanzania kuanza majadiliano na maafisa wa Serikali kwa ajili ya kufikia makubaliano ya namna ya kuifanyia marekebisho sheria ya huduma ya vyombo vya habari ya mwaka 2016.
Sheria hiyo, ambayo tangu kupitishwa kwake inatajwa kuwa mwiba kutokana na baadhi ya vipengele kubana uhuru wa vyombo vya habari, huenda ikafanyiwa marekebisho katika miezi ya hivi karibuni baada ya Serikali kuonesha nia na kufanya majadiliano na Viongozi wa wanahabari likiwemo Jukwaa la Wahariri (TEF).
Nape: Wanahabari wanaweza kujisimamia
Hata hivyo, Waandishi wengi wa habari wanasema wamejikuta katika wakati mgumu kutekeleza baadhi ya majukumu yao kutokana na sheria hiyo, lakini sasa wanaanza kuwa na matumaini kutokana na vuguvugu lililoanza la mijadala ya maboresho ya sheria hizo.
Ameongeza kuwa, japo pande hizo bado zimeshindwa kuafikiana katika baadhi ya vipenegele lakini ana imani kuwa katika awamu ya pili ya majadiliano mambo yatakuwa sawa kwani kupitia maongezi ni wazi kuwa Serikali na Waandhishi watafikia muafana weny mtizamo chanya.
Mwandishi, Sabina Martin anasema, “Hii italeta ahueni na wengi wetu sasa angalau tunapata morali kuoka mambo yanaelekea kuiva, tuna imani vyombo vyetu vinavyotuongoza vitasimama kidete kutetea mashali na kupendekeza sheria rafiki katika utendaji wetu wa kazi.”
Wanahabari watakiwa kuzifahamu sheria za Habari
Moja ya mambo yanayotajwa kuwa ya kupigiwa mfano wakati ilipochukua hatua za oungozi Rais Samia Suluhu Hassan ni kuashiria nia ya kutaka uhuru wa vyombo vya habari, akizingulia televisheni za mtandao na magazeti kadhaa ambayo leseni zake zilifutiliwa mbali.
Awali, akiongea katika majadiliano na marafiki wa vyombo vya Habari, Mwandishi Abdul Kanduru amesema, “Nilisikia Mwenyekiti wa jukwaa la wahariri, Deudatus Balile akisema pande hizo mbili zimeafikiana kuviondoa baadhi ya vipengele visivyo na mashiko.”
Kanduru amesema, hakuna haja ya kuendelea kuviweka vipengele vya sheria ambavyo havina mantiki ya kuendelea kuwepo ndani ya sheria hiyo na kwamba ni vyema watunga sera na sheria wakawa makini kwa kuangalia mbali zaidi kwakua uamuzi wao hujuisha Taifa zima.
Majadiliano ya mabadiliko ya Sheria ya Habari, yamekuwa yakiwahusisha baadhi ya viongozi wa jukwaa la wahariri, maafisa wa serikali kutoka Wizara ya habari, mawasialiano na teknolojia ya habari pamoja na ofisi ya mwanasheria wa serikali na yameridhia baadhi ya vipengele kwenye sheria hiyo ili vifanyiwe marekebisho.