Serikali Nchini Urusi, imesema imepeleka Madakati wa dharura 35 pamoja na misaada katika eneo la mashariki mwa Libya, kufuatia Taifa hilo kukumbwa na mafuriko makubwa wiki iliyopita.
Taarifa ya Wizara ya Masuala ya Dharura ya Urusi, imesema Ndege ya tatu iliyokuwa na Madaktari wabobezi imekwishatua Libya ikiwa na karibu watumishi 35 wa wizara hiyo watakaotoa huduma za afya kwa waathirika.
Aidha, tayari pia Urusi imepeleka Hospitali za kuhamishika zenye vyumba vya upasuaji na huduma za uangalizi maalumu.
Madaktari hao 35 watatoa huduma maalumu za tiba kwa hadi watu 100 kwa siku kwenye maeneo ya wahanga.