Vyombo vya Usalama nchini DCR vinasema zaidi ya watu 5,500 bado hawajulikani waliko katika eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya  Kidemokrasia ya Kongo, ambako mafuriko yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 400.

Huku tarifa hiyo ikitolewa, miili ya watu wengi imepatikana katika vijiji vya Bushushu na Nyamukubi katika jimbo la Kivu Kusini, eneo la Kalehe, tangu mvua kubwa iliyonyesha kusababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi yaliyoharibu majengo na mazao shambani.

Aidha, wengi wa waliofariki ni wanawake na watoto, ambao kwa pamoja walizikwa kwenye makaburi ya halaiki jambo lililozua malalamiko kutoka kwa baadhi ya asasi za kiraia wakisema maziko hayo hayakuwa na heshima.

Wafanyakazi wa Shirika la Msalaba Mwekundu wametoa tahadhari kuhusu ukosefu wa vifaa vya kuwasaidia zaidi ya wakazi 8,800 walioathirika, wengi wao wakiwa wameachwa bila makazi kutokana na maafa hayo mabaya zaidi katika historia ya hivi karibuni ya DRC.

Matukio Wachungaji tata: Yesu wa Kenya ajipeleka Polisi
Mpole ambariki Mayele, amkataa Baleke